CWT NSIMBO WAMEFANYA UCHAGUZI WAWAKILISHI MAHALA PA KAZI,NAFASI YA WENYE ULEMAVU KAMA KAWAIDA
Na.Issack Gerald-Katavi
WALIMU wanne akiwemo Onorine Boniface
mwakilishi wa walimu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamechaguliwa
kuwakilisha walimu wenzao katika chama CWT ndani ya halmashauri hiyo wakitoka
katika shule wanazofundisha.
Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Hamis
Ismail ambaye ni katibu wa chama cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi
amewataja wengine waliochaguliwa kuwa ni Nelson Mwangole na Amani Shaban kwa
upande wa shule za sekondari huku Essa Kyendesya akiwa shule ya msingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama
cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi John Mshota ametoa wito kwa
waliochaguliwa kuwa wawakilishi kwa kuunganisha walimu kuwa kitu kimoja ili
kujenga mshikamano.
Walimu ambao wamechaguliwa wameahidi
kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na walimu wanachama ili kuhakikisha
wajibu,haki na maslahi ya chama yanalindwa kwa manufaa ya chama na taifa.
Wakati huo huo,katibu wa chama cha
walimu Tanzania CWT Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,amesema uchaguzi wa nafasi
ya mwenyekiti wa chama cha CWT katika Halmashauri hiyo iliyoachwa wazi baada ya
mwenyekiti Kenedy Simsokwe kujiudhuru wadhifa huo itatangazwa baadaye.
Aidha Mw.Mshanga amewataka viongozi 4
wapya waliochaguliwa kutoka shule za sekondari na msingi,kuachia nafasi moja ya
uongozi kwa mwenye nafasi zaidi ya mbili huku akiagiza uchaguzi ufanyike kabla
ya mwezi Oktoba kukamilika ili kupata viongozi watakaosimamia shughuli za chama
katika kituo cha kazi ili kuziba pengo litakalokuwa limepatikana.
Comments