MAJOPKOFU YA KUHIFADHIA MAITI MKOANI RUKWA ZAIDI YA WEZI HAYAFANYI KAZI.
MAJOKOFU
ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Rukwa
yameharibiribika kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka sasa.
Kaimu
Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Emanuel Matika,amekiri
kuharibika kwa majokofu hayo ambapo amesema wao kama uongozi wametoa taarifa
TEMESA lakini kwa kuwa hawanafedha ndiyo maana mpaka sasa hayajatengenezwa.
Kwa
mjibu wa Dkt.Matika,utaratibu wa sasa uliowekwa na TEMESA ni lazima walipwe
fedha ndipo watengeneze na ambapo wanaendelea na mchakato wa kutafuta fedha ili
majokofu yatengenezwe.
Katika
hatua nyingine Dk Mtika kutokana na kuharibika kwa majokofu hayo kwa ndugu wanaosafirisha
miili ya ndugu zao wanatumia dawa aina ya fomalini ili kuitunza
isiharibike.
Mmoja
wa wakazi wa mji wa Sumbawanga Maria Kayanda ambaye mjomba wake alifariki dunia
Siku chache zilizopita alisema walilazimika kufanya maziko haraka kutokana na
kushindwa kupeleka mwili wa mjomba wake huyo baada ya kupata taarifa kuwa
majokofu ya chumba cha kutunzia maiti yameharibika.
Alisema
mjomba wake alifariki usiku na wakafanya maziko siku iliyofuata lakini wao
walitamani kuwasubiri ndugu zao wengine waliopo nje ya mji wa Sumbawanga na
mkoa wa Rukwa lakini walishindwa na hivyo kulazimika kuzika.
Kutokana
na hali hiyo kumeleta usumbufu na gharama kwa baadhi ya ndugu wa marehemu ambao
wanapenda kuhifadhi miili ya marehemu ili kuwasubiri ndugu wengine waliombali
wafike kwa ajili ya kuhudhuria maziko.
Comments