MASHEHE 5 MKOANI KATAVI WAMEJIUZURU
Na.Issack Gerald Mashehe watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari wamesema kujizulu kwao ni kutokana na shehe wa Mkoa wa Katavi kukiuka Katiba ya Bakwata. Katika picha ni Shehe Mashaka Kakulukulu miongoni mwa waliojiuzuru Wajumbe waliojiuzulu wakiwemo Mashehe Mohamad Shaaban Sigulu na Said Haruna Omary wamemtuhumu Shehe wa Mkoa Ally Hussein kuwa kinara wa kukiuka kat iba ya Bakwata. Wajumbe wengine wa baraza la mashehe Mkoa waliojiuzuru ujumbe ni Shehe Mashaka Nassoro Kakulukulu na Hassan Mbaruku. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoani Katavi Shehe Shaban Bakari ambaye naye juzi amejiuzuru,amesema Shehe wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein amekuwa akizuia maendeleo ya dini ya kiislamu kwa kutokubaliana na maamuzi ya vikao halali huku akiunga mkono waharifu na wanaopinga maendeleo ndani ya dini. Aidha Shehe Bakari amesema sababu nyingine ambayo imewafanya wajiuzuru ni baada ya shehe...