MWANAFUNZI AUAWAWA KIKATIRI POLISI KATAVI WAMSAKA MUUWAJI
Na.Issack Gerald-Katavi JESHI la polisi mkoani Katavi linamsaka mtu asijejulikana kwa tuhuma za kumbaka,kumchoma kisu,kumuua na kisha kukata sehemu za siri za mwanafunzi(14) wa darasa la sita shule ya msingi Vikonge wilaya ya Tanganyika na kukimbilia kusiko julikana. Akitoa taarifa ya tukio hilo kamanda wa polisi Damas Nyanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 1;30 za asubuhi wakati marehemu akiwa anakwenda shule akiwa ameongozana na mdogo wake ambaye wanasoma shule moja. Alisema kuwa siku ya tukio hilo marehemu alitoka nyumbani akiwa na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la nne ambaye waliongozana wakielekea shule ya msingi vikonge ambayo wanasoma. Kamanda Nyanda alisema wakiwa njiani alitokea mwendesha pikipiki maarufu kwa jina bodaboda ambae walikuwa hawamfahamu na kusimamisha...