MWANAFUNZI AUAWAWA KIKATIRI POLISI KATAVI WAMSAKA MUUWAJI
Na.Issack Gerald-Katavi
JESHI
la polisi mkoani Katavi linamsaka mtu asijejulikana kwa tuhuma za kumbaka,kumchoma
kisu,kumuua na kisha kukata sehemu za siri za mwanafunzi(14) wa darasa la
sita shule ya msingi Vikonge wilaya ya Tanganyika na kukimbilia
kusiko julikana.
Akitoa
taarifa ya tukio hilo kamanda wa polisi Damas Nyanda alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi majira ya saa 1;30 za asubuhi wakati marehemu akiwa anakwenda
shule akiwa ameongozana na mdogo wake ambaye wanasoma shule moja.
Alisema
kuwa siku ya tukio hilo marehemu alitoka nyumbani akiwa na
mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa
darasa la nne ambaye waliongozana
wakielekea shule ya msingi vikonge ambayo wanasoma.
Kamanda Nyanda alisema wakiwa njiani alitokea mwendesha pikipiki maarufu kwa jina bodaboda ambae walikuwa hawamfahamu na kusimamisha pikipiki yake na kuwaambia anataka awape lifti ili wafike haraka shuleni kwao.
Kamanda Nyanda alisema wakiwa njiani alitokea mwendesha pikipiki maarufu kwa jina bodaboda ambae walikuwa hawamfahamu na kusimamisha pikipiki yake na kuwaambia anataka awape lifti ili wafike haraka shuleni kwao.
Alisema
baada ya kuambiwa hivyo wanafunzi hao walikubali
hata hivyo alimtaka apande kwenye bodaboda hiyo mtoto huyo wa kike peke
yake na aliondoka na kumwacha mdogo wake wa kiume.
Baada
ya kunyimwa lifti hiyo mdogo wake aliamua kutembea kufuata nyuma hata hivyo
akiwa njiani aliona pikipiki kama ile
iliyokuwa imembeba dada yake ikiwa kwenye kichaka pembeni ya
barabara lakini hakwenda kuangalia badala yake aliendelea na
safari yake ya kwenda shule.
Mdogo
wake huyo na marehemu kutokana na umri kuwa mdogo alipofika
shuleni hakumtafuta dada yake na badala yake
aliingia darasani na kuendelea na masomo
kama kawaida na baada ya muda wa
masomo ulipofikia majira ya saa 8;30 alianza
safari ya kurejea nyumbani pasipo kumtafuta dada yake.
Kamanda
Nyanda alieleza kuwa baada ya kufika nyumbani kwao
wazazi wake walishituka kumwona akiwa peke yake
ndipo walipomuuliza aliko dada yake
na aliwaeleza mazingira yote ya jinsi
alivyo achana na dada yake wakati walipokuwa
njiani na jinsi alivyoiona pikipiki iliyombeba
dada yake ilivyokuwa kichakani.
Wazazi
wa marehemu baada ya kupata maelezo hayo walipatwa
na mashaka ambapo walimtaka mdogo wa marehemu
awapeleke kwenye eneo aliloona pikipiki ile.
Alisema
wazazi wa marehemu waliokuwa wameongozana na majirani zao baada ya
kufika kwenye eneo hilo walishitushwa kuona
majani yakiwa yamelala na ndipo walipokwenda mbele
kidogo wali ukuta mwili wa marehemu ukiwa amechomwa
kifu sehemu ya ubabu wake wa kulia na sehemu za
siri zikiwa zimenyofolewa.
Kwaupande
wake kaimu mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Vikonge Gadinendi Kaseka
alisema mpaka walipomaliza masomo ya
siku hiyo hawakuwa na taarifa juu ya kifo cha mwanafunzi huyo
ila walipata taarifa hiyo siku hiyo hiyo majira ya saa kumi
na mbili jioni baada ya mwili wa marehemu kuwa umepatikana.
Kamanda
huyo wa polisi alisema kuwa wazazi na majirani walikwenda polisi kutoa
taarifa ambapo polisi walifika na kuuchukua mwili wa marehemu na msako wa mtu
aliyefanya tukio hilo unaendelea.
Habari zaidi ni
kupitia P5TANZANIA LIMITED
Comments