RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO
SERIKALI mkuu mkoani Rukwa imepiga marufuku kuutumia mwalo uliopo katika Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafisirisha kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika. Alisema kuwa wananchi wasipotoshe lengo la kutebnwa kwa mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na si kwaajili ya magari kupakilia mizigo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na kubore...