WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WASITISHA MGOMO WA SIKU MBILI
Mamia ya wafanyabiasahara katika
masoko ya Mpanda Mkoani Katavi leo wameanza kufanya biashara kama kawaida
kufuatia kuwepo kwa mgomo huo kwa muda wa siku mbili.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wamesema wamefanya mazungumzo na uongonzi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani
Katavi ili kufikia mwafaka wa mgomo uliosababishwa na kupandishwa kwa bei ya
Pango kutoka sh 15,000 kwa hapo awali na kufikia shilingi 60,000.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko la
Buzogwe ambalo ni kitovu cha mvutano huo Bw.Ramadhani Karata amedai amekuwa mafichoni
kwa muda kutokana na kuandamwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za yeye
kuwa chanzo.
Mgomo wa wafanyabiashara hasa katika
soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe ulianza juzi ambapo Mkuu wa
Wilaya alikuwa amesisitiza kuwa mfanyabiashara asiyetaka kulipa tozo hizo
arudishe chumba cha biashara.
Hata hivyo mwafaka kamili kuhusu kiasi
ambacho kinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara kinatarajiwa kutolewa baada ya
wiki moja hiyo ikiwa ni kwa mjibu wa maazimio yaliyoafikiwa katika mkutano
ulioendeshwa na Chama cha CCM Mkoani Katavi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments