RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO
SERIKALI mkuu mkoani Rukwa imepiga marufuku kuutumia mwalo uliopo katika Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili
ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za
kuuzia samaki.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo
alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo
wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia
mizigo kwa lengo la kusafisirisha
kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika.
Alisema kuwa wananchi wasipotoshe
lengo la kutebnwa kwa mwalo huo ambayo
ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na
si kwaajili ya magari kupakilia mizigo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu
iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha
ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo
jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na
kuboresha.
Awali kabla ya Kukaribishwa Mkuu wa
Mkoa, Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy alikemea vitendo vya wananchi wa
Kirando kutumia mwalo huo kama bandari jambo ambalo ni kinyume na sheria na
kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Nkasi Said Mtanda aliwaasa wananchi wanaotumia vyombo usafiri ziwani kuzingatia
kuvaa maboya na kuonya kutozidisha mizigo na abiria na kuwasisitiza wasafiri wa
majini kuwa watumiaji wawe wantoa taarifa endapo wataona taratibu zinakiukwa
kwakuwa wasafirishaji hao huangalia faida kuliko usalama wa maisha ya abiria
wao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments