Katika picha,Wa tatu kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga akisikiliza maelezo kuhusu kiwanda kutoka kwa mwenyekiti wa Kashaulili Livestock Keepers Bw.Andrea Fumbi(wa pili kutoka kushoto) (Picha na P5tanzania.blogspot.com) Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya Makakanyagio Halmashauli ya Manispaa Mpanda. Jiwe la Msingi katika mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio kinapojengwa kiwanda cha kuzalisha maziwa Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benky...