KITUO CHA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU MPANDA WAOMBA MSAADA KUKIDHI MAHITAJI YAO MUHIMU-Julai 19,2017
KITUO cha Gethsemani cha kulelea
watoto wanaoishi
katika mazingira magumu kilichopo kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya Nsimbo
Mkoani Katavi,kimeomba mchango wa hali na mali kutoka kwa jamii ili kupata pesa
kukidhi mahitaji muhimu ya watoto wanaoishi katika kituo hicho.
Msimamizi wa
kituo hicho Bw.Godfred Stephano ametoa ombi hilo leo katika mahojiano na
waandishi wa habari.
Aidha
Bw.Stephano ameiomba jamii kushirikiana kwa pamoja katika ujenzi wa mabweni ya wasichana na wavulana
ambapo August 8 mwaka huu wanatarajia kuendesha zoezi la uchangishaji ili
kupata fedha ya kujengea mabweni hayo.
Hata
hivyo,baadhi ya wadau wamekuwa wakijitolea na kuwachangia watoto ambapo Kituo
cha Gethsemani mpaka
kufikia mwaka jana kilikuwa na watoto zaidi100.
Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi
Comments