MKUU WA MKOA WA KATAVI MEJA JENERAL MSTAAFU RAFAEL MUHUGA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA KUZALISHA MAZIWA MKOANI KATAVI-Julai 19,2017
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka
jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha
Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya
Makakanyagio Halmashauli ya Manispaa
Mpanda.
Jiwe la Msingi katika mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio kinapojengwa kiwanda cha kuzalisha maziwa |
Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi
kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda
kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda
hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho
kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benkya TIB,ambapo kinatarajia
kuzalisha maziwa ifikapo September mwaka huu.
Wakati huo huo Afisa mazingira
Manispaa ya Mpanda Bw.Said Mandua pamoja na mambo mengine amewatoa hofu usalama
wa mazingira katika makazi wakazi wa Manispaa ya Mpanda kutokana ujenzi wa
kiwanda hicho ambacho kipo nje kidogo ya mita 60 kutoka chanzo cha mto Mpanda.
Mpaka sasa Mkoa wa Katavi una viwanda
viwili vya maziwa ambapo kimoja kilichopo
kata ya Ilembo kilizinduliwa na na mwenge wa uhuru mwezi April mwaka huu.
Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi
Comments