Posts

Showing posts from December 21, 2017

TMA IMETAJA MIKOA ITAKAYOPATA MVUA KUBWA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWISHO WA MWAKA

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka,mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya,Songwe,rukwa na Kigoma. Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA,Samuel Mbuya,amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli. Mbuya alieleza Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu huku mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni. Aidha amesema TMA inatarajia mvua zitaendelea kunyesha katika mikoa ya Kigoma,tabora,Katavi,Rukwa, Songwe,Mbeya,Ruvuma,Lindi,Dodoma na Singida. Mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili mwakani. Wakati huo huo Mbuya amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA mara kwa mara ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na k...

JELA MIAKA 30 KWA KUUA TEMBO MKOANI KATAVI

Image
MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Jackison  Eijuel (52) mkazi wa kata ya Katumba kutumikia kifungo cha  miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99 baada ya kupatikana na  hatia ya kumiliki na meno manne ya tembo pamoja na vipande vinne vya meno hayo. Hukumu  hiyo  ilitolewa juzi  na  hakimu   mkazi  mfawidhi wa  mahakama hiyo Chiganga  Tengwa baada ya  kuridhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo  ambapo mshitakiwa  hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake. Akisoma hukumu  hiyo hakimu Twengwa alisema  mahakama imebaini mtuhumiwa alitenda kosa hilo  kinyume  na  kifungu  cha  sheria  namba 235  cha mwenendo  wa  mashitaka. Alisema  baada ya  kusikiliza  ut...