JELA MIAKA 30 KWA KUUA TEMBO MKOANI KATAVI
MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu
Jackison Eijuel (52) mkazi wa kata ya Katumba kutumikia kifungo
cha miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99 baada ya
kupatikana na hatia ya kumiliki na meno manne ya tembo pamoja na
vipande vinne vya meno hayo.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na
hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo
Chiganga Tengwa baada
ya kuridhika na ushahidi
uliotolewa Mahakamani hapo ambapo
mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Twengwa alisema
mahakama imebaini mtuhumiwa alitenda kosa hilo
kinyume na kifungu cha
sheria namba 235 cha
mwenendo wa mashitaka.
Alisema baada
ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa ,mahakama imethibisha
pasipo kuacha shaka
yoyote kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia
kwa kukamatwa akiwa na meno ya tembo
ambayo ni sawa tembo watatu waliouawa wenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 90.
Awali mwendesha mashitaka
mwanasheria wa Serikali
Fraviani Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa
Jackisoni Elijuel aliyepewa uraia wa Tanzania ambapo awali alikuwa
raia wa Burundi alitenda kosa hilo
Oktoba 25 mwaka huu majira ya saa mbili
na nusu usiku katika Kijiji cha
Urwila tarafa ya Nsimbo wilayani Mpanda.
Shiyo aliiambia mahakama hiyo
kuwa mshitakiwa alikamatwa na
askari maalumu wa kuzuia ujangili
wa pori la Ugala baada ya kupata taarifa
za mshitakiwa kujihusisha na biashara haramu
ya kuuza meno ya tembo.
Aidha Shiyo alieleza kuwa baada ya askari hao kupata taarifa hizo ndipo walipoandaa mtego
na kumkamata
akiwa na meno ya tembo
manne mazima na vipande vinne
vyenye uzito wa kiligramu 27 yenye thamani
ya shilingi milioni 99 ambayo ni sawa na
tembo watatu wazima.
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba
mahakama imwachie huru
kwa kile alichodai kuwa meno
ya tembo aliyokamatwa nayo hayakuwa yake bali
yalikuwa ni ya mtu mmoja aliyemtaja
kwa jina la Hussen Samora kuwa ndiye aliyekuwa amemtuma
kuyabeba kwa kutumia pikipiki yake mshitakiwa ili
ampelekee.
Baada ya utetezi huo kabla ya
hakimu kusoma hukumu wakiri wa Serikali Shiyo aliiomba
mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili
iwe fundisho kwa
watu wengine kwani vitendo
vya ujangili vimezidi kushamili katika hifadhi ya Katavi.
Baada
ya kuusikiliza utetezi wa mshitakiwa
hakimu huyo wa alimtaka mshitakiwa ataje
namba za pikipiki ambayo alidai
ni mali
yake aliyoitumia kubebea meno hayo
ya tembo
na amekuwa akiiendesha kwa
kipindi cha miaka miwili hata hivyo
mshitakiwa alishindwa
kuzitaja namba hizo za
pikipiki aliyodai ni ya kwake kitendo
kilichothibitisha aliidanganya mahakama kuwa alikodiwa ili pikipiki yake
itumike kubeba meno hayo ya tembo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Tengwa
alisema mshitakiwa amekutwa na hatia
kinyume na kifungu cha sheria namba 235
ya mwenendo wa mashitaka hivyo mahakama imemuhukumu
kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya
shilingi milioni 99.
Habarika zaidi na P5TANZANIA LIMITED
Comments