TMA IMETAJA MIKOA ITAKAYOPATA MVUA KUBWA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWISHO WA MWAKA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka,mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya,Songwe,rukwa na Kigoma.
Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA,Samuel Mbuya,amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli.
Mbuya alieleza Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu huku mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni.
Aidha amesema TMA inatarajia mvua zitaendelea kunyesha katika mikoa ya Kigoma,tabora,Katavi,Rukwa, Songwe,Mbeya,Ruvuma,Lindi,Dodoma na Singida.
Mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili mwakani.
Wakati huo huo Mbuya amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA mara kwa mara ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na kuchukua tahadhari mapema.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA