Posts

Showing posts from January 15, 2018

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA KAGERA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kufuatia watu 11 kupoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Nyangozi, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera. Ajali hii imetokea jana baada ya basi dogo la abiria aina ya Nissan Caravan lililokuwa likitoka Kakonko Mkoani Kigoma kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga kuligonga ubavuni lori la mizigo kisha kugongana uso kwa uso na lori jingine na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 6 kujeruhiwa. Mhe.Rais Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Watanzania hao na amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kumfikishia pole kwa familia za Marehemu wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo. Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wa barabara hasa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na ameviagiza vyombo vin...

LOWASSA AANIKA ALICHOZUNGUMZA NA RAIS MAGUFULI IKULU

Image
Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania,CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita. Katika  Haki miliki ya picha IKULU Image caption Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015 taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Chama cha Demokrasia na Maendeleo,imenuukuu ujumbe wa Lowasa ukieleza kuwa  Rais Magufuli alimshawishi arudi na kujiunga na CCM jambo ambalo hakukubaliana nalo. Wiki iliyopita,kiongozi huyo wa upinzani nchini ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, amekutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya. Lowassa aliwania urais kupitia chama kikuu  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

UJENZI WA VYOO VYA SOKO KUANZA NSIMBO,MWENYEKITI WA HALAMSHAURI AONYA

Ujenzi wa vyoo katika soko la Mnyaki kata ya Katumba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,unatarajiwa kuanza kesho baada ya muda mrefu eneo hilo kukosa vyoo. Mwenyekiti wa soko la hilo Leonard Kigwasu amesema  ujenzi huo unaanza kutokana na kukamilika zoezi la ukusanyaji wa fedha. Aidha Kigwasu ameiomba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika soko hilo ili kuboresha hali ya usafi. Kauli hiyo inapingana na Kauli aliyoitoa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya nsimbo Rafael Kalinga ambaye amekanusha uwepo wa mchango wa ujenzi wa vyoo na kuahidi kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kuchukua hatua endapo kutakuwa na ukiukwaji wa taratibu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO AFAFANUA UKOSEFU WA DIWANI KATA YA KATUMBA

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh . Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu Kata ya Katumba katika halmashauri hiyo kutokuwa na Diwani tangu mwaka jana. Akizungumza mapema leo amesema halmashauri inajipanga kwenda katika kata hiyo ili kukutana na watendaji wakiwemo wananchi ili waendelee kutoa ushirikiano kwa diwani wa viti maalumu. Katika hatua nyingine amesema wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu kujua hatima ya suala hilo. Siku ya jana Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh . Rhoda Kunchela amesema kitendo cha wananchi wa kata hiyo kukosa Diwani hakikubaliki kwani kinadhoofisha jitihada za maendeleo  ya wananchi. Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka alifungwa mwaka jana miaka 3 jera  kwa kosa la kupokea rushwa kwa mfugaji wa kata hiyo ili amuidhinishie eneo la kufugia ambalo limepigwa marufuku na Mahakama. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

AJALI YAU 11 YAJERUHI WENGINE MKOANI KAGERA

Image
Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya H i a ce kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilaya ni Biharamulo mkoani Kagera usiku wa kuamkia . Gari hiyo yenye namba za usajil T.542 DKE ilikuwa ikitokea Wilaya ni Kibondo kuelekea Kahama mkoani Shinyanga huku maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo yakiwa  chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi. Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na idadi hiyo ya vifo na kwamba taarifa zaidi na majina itatolewa baada ya muda mfupi ili kutambua majina ya waliopoteza maisha Naye Mganga Mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr . Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED