MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO AFAFANUA UKOSEFU WA DIWANI KATA YA KATUMBA
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh.Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu Kata ya Katumba katika halmashauri hiyo kutokuwa na Diwani tangu mwaka jana.
Akizungumza
mapema leo amesema halmashauri inajipanga kwenda katika kata hiyo ili kukutana
na watendaji wakiwemo wananchi ili waendelee kutoa ushirikiano kwa diwani wa
viti maalumu.
Katika
hatua nyingine amesema wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu kujua hatima ya
suala hilo.
Siku ya
jana Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia
na maendeleo Chadema Mh.Rhoda
Kunchela amesema kitendo cha wananchi wa kata hiyo kukosa Diwani hakikubaliki
kwani kinadhoofisha jitihada za maendeleo ya wananchi.
Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka alifungwa
mwaka jana miaka 3 jera kwa kosa la kupokea rushwa kwa mfugaji wa kata
hiyo ili amuidhinishie eneo la kufugia ambalo limepigwa marufuku na Mahakama.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments