UJENZI WA VYOO VYA SOKO KUANZA NSIMBO,MWENYEKITI WA HALAMSHAURI AONYA
Ujenzi wa vyoo katika soko la Mnyaki kata ya Katumba Halmashauri ya
wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,unatarajiwa kuanza kesho baada ya muda mrefu
eneo hilo kukosa vyoo.
Mwenyekiti wa soko la hilo Leonard Kigwasu amesema ujenzi huo
unaanza kutokana na kukamilika zoezi la ukusanyaji wa fedha.
Aidha Kigwasu ameiomba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kusaidia
upatikanaji wa huduma ya maji katika soko hilo ili kuboresha hali ya usafi.
Kauli hiyo inapingana na Kauli aliyoitoa mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya nsimbo Rafael Kalinga ambaye amekanusha uwepo wa mchango wa ujenzi wa
vyoo na kuahidi kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kuchukua hatua endapo
kutakuwa na ukiukwaji wa taratibu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments