LOWASSA AANIKA ALICHOZUNGUMZA NA RAIS MAGUFULI IKULU
Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania,CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita.
Katika
IKULU
Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015 taarifa iliyotolewa
kwa waandishi wa habari na Chama cha Demokrasia na Maendeleo,imenuukuu ujumbe
wa Lowasa ukieleza kuwa Rais Magufuli
alimshawishi arudi na kujiunga na CCM jambo ambalo hakukubaliana nalo.
Wiki iliyopita,kiongozi
huyo wa upinzani nchini ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, amekutana na Rais
wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.
Lowassa aliwania urais
kupitia chama kikuu Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na
Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments