AJALI YAU 11 YAJERUHI WENGINE MKOANI KAGERA
Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya Hiace kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilayani Biharamulo mkoani Kagera usiku wa kuamkia.
Gari hiyo yenye namba za
usajil T.542 DKE ilikuwa ikitokea Wilayani Kibondo
kuelekea Kahama mkoani Shinyanga huku maroli
yaliyohusika kwenye ajali hiyo yakiwa chini ya usalama wa jeshi la polisi
kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na idadi hiyo
ya vifo na kwamba taarifa zaidi na majina itatolewa
baada ya muda mfupi ili kutambua majina ya waliopoteza maisha
Naye Mganga Mkuu wa
hospitali teule ya Biharamulo Dr.Grasmus Sebuyoya
amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa
jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments