Posts

Showing posts from November 11, 2017

LORI NOAH ZAUA 5 NA KUERUHI 4 MKOANI KILIMANJARO

Na.Issack Gerald Watu watano Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamepoteza maisha na wengine wanne wakijeruhiwa. Aajali hiyo ambayo imehusisha lori kugongana uso kwa uso na Noah imetokea maeneo ya kikavu kwa Sadala. Daktari wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano. Aidha Dkt.Temba amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai. Kwa upande wa majeruhi Dkt.Temba amesema wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RIPOTI KAMILI YA MAHAKAMA KUU SAKATA LA CUF HII HAPA

Image
MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi juu ya Maombi ya Zuio dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri dogo la madai [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2 kutoka Mahakama Kuu ni kama ifuatavyo; 1.Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. 2.Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF [Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote KUJADILI juu ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. 3.Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF [WAPELEKA MAOMBI -APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI YAO ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO YALIYOWASILISHWA MBELE YAKE. 4.Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliwekwa na Lipumba na ...

WATENDAJI WALIOGAWA MAENEO KWA WANANCHI KIHOLELA KUCHUKULIWA HATUA

Image
Serikali imeziagiza halmashauri nchini kuanza kuchukua hatua kwa watendaji walio husika kugawa maeneo ya makazi kwa wananchi kiholela. Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na Makazi Anjerina Mabula alipokuwa akijibu maswali yaliyo ulizwa na baadhi ya wabunge walio taka kujua kwanini serikali inaadhibu wananchi kwa kubomoa makazi yao na kuwaacha watendaji walio idhinisha. Ameongeza kusema kuwa hatua zinachukuliwa na serikali kuhakikisha hakuna uonevu dhidi ya wananchi. Nisiku ya  tatu tangu mkutano wa tisa wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kwake mjini Dodoma. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED