WATENDAJI WALIOGAWA MAENEO KWA WANANCHI KIHOLELA KUCHUKULIWA HATUA
Serikali imeziagiza halmashauri nchini kuanza kuchukua hatua kwa
watendaji walio husika kugawa maeneo ya makazi kwa wananchi kiholela.
Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na
Makazi Anjerina Mabula alipokuwa akijibu maswali yaliyo ulizwa na baadhi ya
wabunge walio taka kujua kwanini serikali inaadhibu wananchi kwa kubomoa makazi
yao na kuwaacha watendaji walio idhinisha.
Ameongeza kusema kuwa hatua zinachukuliwa na serikali kuhakikisha hakuna
uonevu dhidi ya wananchi.
Nisiku ya tatu tangu mkutano wa tisa wa bunge la jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kuanza kwake mjini Dodoma.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments