LORI NOAH ZAUA 5 NA KUERUHI 4 MKOANI KILIMANJARO
Na.Issack Gerald
Watu watano Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamepoteza maisha na
wengine wanne wakijeruhiwa.
Aajali hiyo ambayo imehusisha lori kugongana uso kwa uso na Noah
imetokea maeneo ya kikavu kwa Sadala.
Daktari wa zamu katika
hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano.
Aidha Dkt.Temba amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika
hospitali ya wilaya ya Hai.
Kwa upande wa majeruhi Dkt.Temba amesema wamekimbizwa katika
hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments