RIPOTI KAMILI YA MAHAKAMA KUU SAKATA LA CUF HII HAPA
MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi juu ya Maombi ya
Zuio dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri dogo la madai [MISCELLENEOUS
CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2
kutoka Mahakama Kuu ni kama ifuatavyo;
1.Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA
UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
2.Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya
Wadhamini ya CUF [Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote
KUJADILI juu ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
3.Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF
[WAPELEKA MAOMBI -APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI
YAO ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO YALIYOWASILISHWA
MBELE YAKE.
4.Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote
yaliwekwa na Lipumba na Wenzake katika shauri hili.
Haya ndio maamuzi ya msingi yaliyotolewa na MAHAKAMA
KUU. Maamuzi haya tafsiri yake ni kwamba kile alichokifanya SPIKA WA BUNGE Job
Ndugai ni BATILI, NA WABUNGE 8 NA DIWANI 1 WA MANISPAA YA TEMEKE WALIOAPISHWA
NI BATILI KWA KUWA WAHUSIKA WOTE BADO NI WANACHAMA HALALI WA THE CIVIC UNITED
FRONT[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]. NI KWA MSINGI NI HUO Hatua na taratibu za
kisheria zitachukuliwa kuhakikisha kuwa HAKI INAREJESHWA KWA WENYE KUSTAHIKI
NAYO NA WABUNGE WA LIPUMBA WATATOKA BUNGENI.
Aidha, Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za Mwanasheria wa
Manispaa wa Ubungo na Temeke juu ya utaratibu uliotumika Manispaa zao
kufikishwa Mahakamani hapo kuwa haukufuata taratibu za kisheria na kwamba
Mahakama haina Mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuchunguza Maamuzi yaliyofanywa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] kwa Mujibu wa Katiba na Sheria.
MAHAKAMA KUU IMEFUNGUA MLANGO WA KUSHUGHULIKIA Shauri la msingi
(CIVIL CASE NO. 143/2017) Lililopangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 13/2/2017
kati ya Wabunge wetu 8 ambao ndio WADAI [APPLICANTS]
1. MIZA BAKARI HAJI
2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]
3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]
4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]
5. RIZIKI SHAHRI NG'WARI [MBUNGE]
6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]
7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]
8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]
9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA
TEMEKE.
10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA UBUNGO.
DHIDI YA WADAIWA [RESPONDENTS]
1) BODI YA WADHAMINI -CUF,
2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,
3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,
4) MKURUGENZI TUME-NEC,
5) KATIBU WA BUNGE,
6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE
7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO
8) RUKIA AHMED KASSIM,
9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,
10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,
11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,
12) HINDU HAMIS MWENDA,
13) SONIA JUMAA MAGOGO,
14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,
15) NURU AWADH BAFADHILI
HOJA ZA WABUNGE WETU :
1.Wabunge na Madiwani Wetu walikuwa wanadai HAKI YA UANACHAMA
WAO ambayo tayari leo imerejeshwa kwao.
2.Wanahoji jinsi mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya kuwavua
uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi
yanayoendelea mahakamani yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro
uliopandikizwa na Vyombo vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya siasa
nchinji unaoendelea.
3.Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za
nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa
rasmi za tuhuma zao kwa maandishi, siku na tarehe ya kikao hicho, kupata nafasi
ya kujitetea, huku ikizingatia kuwa si wote wanaoishi Dar es Salaam,
kulikofanyika kikao cha maamuzi.
4.Uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua
bila kujiridhisha vyakutosha.
5.Kutokupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kwa mujibu wa
Katiba ya CUF na vikao kuendeshwa kwa speed ya mwendokasi-‘DART'
6.Maamuzi hayakuzingatia haki za kikatiba za mwanachama ikiwemo
haki ya kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, Mkutano
Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya
Chama.
7.Je Vyombo vilivyowachukulia hatua za kinidhamu vina uhalali wa
Kikatiba ndani ya CUF? Hayana mengine mengi ndiyo yanayohojiwa Mahakamani
katika shauri hili la msingi.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Mawakili wetu Wasomi
Peter Kibatara na Omary Msemo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kulisimamia suala
hili kwa weledi mkubwa. Tunawapongeza Viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali za
Chama, Wanachama, Madiwani na Wabunge wote waliokuwa pamoja na CHAMA NA AMBAO
HAWAKUKUBALI KUYUMBA WALA KUYUMBISHWA kwa kufanikisha na kusimamia mapambano
haya ya kisheria. Tunaamini na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwamba HAKI NA USHINDI
VIPO KARIBU KUPATIKANA.
JAJI NDYASOBERA ATOA AMRI YA KUITWA WAJUMBE BODI YA RITA:
Katika hatua nyingine ya mapambano ya kisheria Jumatatu Tarehe
13/11/2017 Mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
FEKI' ya Lipumba wameitwa Mahakama Kuu kwenda kujieleza MMOJA MMOJA juu ya
uhalali wao.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 10/11/2017
Na.Kurugenzi ya Habari,Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
HABARIKA
ZAIDI NI P5TANZANIA LIMITED
Comments