MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA FUNGUZI WA MKUTANO WA 37 WA SADC MJINI PRETORIA-Agosti 19,2017
Viongozi wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.