MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA FUNGUZI WA MKUTANO WA 37 WA SADC MJINI PRETORIA-Agosti 19,2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
leo amehudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria
Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John
Pombe Magufuli.
Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu
majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 – Agosti 2017 kwa niaba ya
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake.
Makamu wa Rais
amewasilisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali taarifa ya utekelezaji wa majukumu
ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 kwa niaba ya
Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa hiyo
inaelezea hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda katika kipindi
tajwa hususan katika Nchi za DRC, Madagascar na Lesotho.
Aidha taarifa hiyo
pia imetoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zinazoendelea kuikabili
Kanda katika maeneo ya siasa, ulinzi na usalama.
Taarifa hiyo pia
imeelezea hali ya demokrasia na chaguzi zilizofanyika kwa kipindi cha 2016/2017
kwa nchi wanachama.
Katika Mkutano huu
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhi Uenyekiti wa Asasi ya SADC
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Angola, baada ya Tanzania
kukamilisha kipindi cha Uongozi wake chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkutano huu wa SADC
uliofunguliwa rasmi leo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyeji
wa Mkutano wa 37 wa SADC, ulitanguliwa na mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Troika Mbili uliofanyika tarehe18 Agosti, 2017
Mkutano wa Troika
Mbiliumefanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama (SADC MCO) uliofanyika Dar es
Salaam tarehe 20 na 21 Julai, 2017 ambapo Mawaziri waliona ipo haja ya kuitisha
Double Troika pembezoni mwa Mkutano huu wa 37 ili kujadili pamoja na mambo
mengine, hali ya ulinzi na usalama.
Troika Mbili
inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika
Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.
Serikali ya Afrika
Kusini ambayo ni mwenyeji wa Mkutano huu wa 37 wa SADC na Mwenyekiti
imependekeza kuwakaulimbiu ya Mkutano wa 37 iwe ni Kushirikiana na Sekta
Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Mfalme Mswati III, Rais wa
Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma amesisitiza nchi wananchama kutekeleza kwa
vitendo Kauli Mbiu ya Mkutano wa 37 wa SADC juu ya kushirikiana na Sekta
Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa kuwa ndio njia
pekee ya nchi za Jumuiya hiyo kupiga hatua kimaendeleo.
Rais Zuma amesisitiza
nchi za Afrika kufanyakazi kwa bidii na kuhakikisha rasilimali za nchi
zinatumika kwa faida ya maendeleo yay a kweli.
Wakuu wa Nchi na
Serikali wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa
SADC 2015 – 2063 ambao ulipitishwa katika Mkutano wa Dharura uliofanyika tarehe
29 Aprili, 2015 mjini Harare, Zimbawe.
Mkakati huu unalenga
kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na kushiriki zaidi
katika mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa na hivyo kuongeza
kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mkutano wa 37 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) utahitimishwa hapo kesho Jumapili tarehe 20
Agosti 2017, kwa kutolewa Tamko (Communique) litakaloelezea yaliyojiri katika
Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali.
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa
Rais
Pretoria, Afrika
Kusini
19 Agosti, 2017.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments