SERIKALI YA TANZANIA YASEMA UJIO WA NDEGE MPYA UKO PALEPALE-Agosti 19,2017
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa |
Kauli ya kuthibitisha
ujio wa ndege hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bi. Zamaradi Kawawa wakati akiongea na
Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Alieleza kuwa
kuchelewa kwa ndege hiyo ambayo ilitakiwa kuwasili mwezi Julai mwaka huu
kumetokana na majadiliano yanayoendelea ambayo kimsingi yamechangiwa na baadhi
ya wanasiasa wasio wazalendo kushiriki kwao moja kwa moja kuweka zuio mpaka
pale majadiliano yatakapo kamilika.
Alieleza kuwa
Serikali iliishapata fununu kuwa kuna kuna baadhi ya viongozi wa chama cha
siasa wana mpango wa kukwamisha juhudi za ujio wa ndege mpya na kwamba bila
hata chembe ya uzalendo, watu hao wamejidhihilisha wenyewe hadharani kwamba
wapo nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali kwa maslahi yao binafsi.
Aidha alisema kuwa
Serikali imeanza kuchukua hatua za diplomasia na za kisheria kwa wote
wanaoshabikia na kutengeneza migogoro na hujuma mbalimbali dhidi ya maendeleo
ya nchi yetu.
Kwa mujibu wa
Zamaradi, kuna wanasiasa waliokwenda kufungua madai kwamba Serikali ya Tanzania
inadaiwa na kwamba ndege hiyo ishikiliwe hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo
na ni vibaraka waliotumwa na wapiga dili wasioitakia mema Tanzania.
Katika siku za hivi
karibuni kumeibuka baadhi ya wanasiasa Watanzania ambao wamekuwa wakitoa kauli
zenye lengo la kuhujumu maendeleo ya nchi ikiwemo kushawishi wafadhili kuinyima
misaada Tanzania lakini pamoja na jitihada hizo, washirika wa maendeleo
wameendelea kuongeza misaada kwa Tanzania kutokana na kuridhishwa na hatua
mbalimbali za Serikali katika kupambana na rushwa na ufisadi na kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments