WANAFUNZI 22 WA SHULE YA SEKONDARI MIRAMBO MKOANI TABORA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUFANYA VURUGU-Agosti 19,2017
JUMLA
ya wanafunzi 22 wa shule ya sekondari Mirambo Mkoani Tabora,wamefikishwa na
kusomewa mashtaka 12 yanayowakabili ikiwemo kufanya vurugu katika kata ya
Chemchemi.
Mwanafunzi
mmoja kati ya hao imelazimika afuatwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora
Kitete na kusomewa mashataka hayo licha ya kuwa alikuwa amelazwa akipatiwa
matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata katika vurugu hizo zilizotokea wiki
iliyopita.
Akisoma
mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Tabora Emanuel Ngigwana,wakili
wa serikali Idd Mgeni ameieleza mahakama kuwa, watuhumiwa wote 22 wanadaiwa
kufanya vurugu kwa kuwajeruhi wananchi na kuharibu mali zao.
Aidha
Wakili mgeni amesema,Agosti 14 mwaka huu majira ya usiku wanafunzi hao
wanadaiwa kuwajeruhi wananchi sita kwa kuwakata na vitu vyenye nchi kali
ikiwemo mapanga na fyekeo ambapo amesema upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika.
Hata
hivyo watuhumiwa wote 22 wamekana kuhusika na wamerudishwa mahabusu baada ya
kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana ambapo ni mwanafunzi mmoja amepata
dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye
bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 31
mwaka huu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments