MKOANI KATAVI AMUUA MKEWE NA KUZIKA MWILI WAKE
Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Songambele Kata ya Sibwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika jina lake limehifadhiwa(45) kwa tuhuma za kumuua mke wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na kisha mzika huku mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akishuhudia tukio. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema tukio la kupatikana kwa mwili wa marehemu huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana katika Kijiji hicho. Alisema marehemu aliuawa na mumewe huyo siku ya januari 15 kwa kupigwa na mumewe kwa kutumia silaha zajadi ambazo ni fimbo na mpini wa jembe baada ...