MKOANI KATAVI AMUUA MKEWE NA KUZIKA MWILI WAKE
Jeshi
la Polisi mkoani Katavi linamshikilia mkazi wa
Kijiji cha Songambele
Kata ya Sibwesa Tarafa ya
Karema Wilaya ya Tanganyika jina
lake limehifadhiwa(45) kwa tuhuma za kumuua mke wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi
na kisha mzika huku mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akishuhudia tukio.
Kamanda wa Jeshi la
Polisi wa mkoa wa
Katavi Damas Nyanda
alisema tukio la kupatikana kwa
mwili wa marehemu
huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana katika Kijiji
hicho.
Alisema marehemu aliuawa na
mumewe huyo siku ya januari
15 kwa
kupigwa na mumewe kwa
kutumia silaha zajadi ambazo ni
fimbo na mpini wa
jembe baada ya kumtuhumu
kuwa anamahusiano wa kimapenzi na wanaume wengine
Kijijini hapo.
Kamanda Nyanda alisema wakati mtuhumiwa huyo akitenda kosa hilo ambalo
lilishuhudiwa na mtoto
wake wa kiume hadi baba yake
alivyomuuawa mama yake
na kisha kuchimba shimo na kumfukia ardhini.
Baada ya kufanya mauaji hayo
na kuzika mwili huo mtuhumiwa alirejea
nyumbani kwake na kuendendelea
na shughuli zake
kama kawaida na alimtishia mtoto wake
huyo mdogo na kumwambia
asimwambie mtu yeyote.
Majirani waliokuwa
wakimfahamu marehemu baada ya
kuona haonekani Kijijini
hapo walianza kumuuliza
mtuhumiwa mahali alipo
mkewe naye alikuwa
akiwajibu kuwa mkewe amesafiri kwenda kwao kusalimia.
Kamanda Nyanda alisema Jeshi la polisi
lilipata taarifa ya mauaji ya
mama huyo hapo
machi 15 na ndipo lilipoanza
uchunguzi wa tukio hilo.
Alileza kuwa baada ya
kufanya uchunguzi wa kina ndipo
juzi walimtia mbaroni
mtuhumiwa na baada ya
mahojiano alikiri kufanya
mauaji hayo kwa kile alichodai kuwa alikasirishwa na tabia ya
mke wake ya kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na wanaume wengine kijijini
hapo na aliwaeleza
polisi kuwa yuko tayari
kwenda kuwaonyesha alipofukia mwili wa
mke wake baada
ya kufanya mauaji.
Baada ya mahojiano
hayo hapo juzi majira ya saa
6;00 mchana polisi walifika kwenye
eneo ambalo mtuhumiwa alikuwa amemfukia
marehemu mkewe na baada ya kufukua eneo
hilo walikuta mwili na kuutambua
kuwa ni mwili wa mwanamke huyo na kisha
kuutoa katika eneo hilo.
Kamanda Nyanda
alisema mwili wa marehemu baada ya kufukuliwa ulichukuliwa na kupelekwa katika
chumba cha kuhifadhi maiti katika Manispaa ya Mpanda.
Mtuhumiwa anaendelea
kushikiliwa na jeshi la
polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika anatarajiwa kufikishwa mahakamani
ili akajibu tuhuma zinazo
mkabili.
Habario zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments