RUKWA BADO WALIA NA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA
MKOA wa Rukwa bado unakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo jumla ya vyumba 4,226 vinakitajika ili kumaliza tatizo hilo. Afisa elimu mkoa huo Nestory Mroka alisema mahitaji hayo yamekuwa yakisababisha mkoa huo kutopiga hatua katika mafanikio ya elimu. Alisema ili wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao ni lazima kuwe na miundombinu mizuri,walimu wa kutosha,vitabu pamoja na walimu lakini kama kuna mapungufu kati ya hayo mambo hata ufaulu hauwezi kuwa mzuri. Aidha Mroka alisema kutokana na changamoto hizo jitihada za makusudi zinahitajika katika kulimaliza tatizo hilo pamoja na mengine ili kuinua ufaulu wa wanufunzi katika shule za msingi pamoja na sekondari ambapo mpaka sasa ufaulu katika kidato cha nne ni wastani wa daraja la nne. Wakati huo huo,Afisa elimu huyo alisema yeye binafsi amejitahidi kuhakikisha anawasimamia walimu ili watimize wajibu wao ipasavyo ikiwamo kuwepo kazini kwa muda mwafaka sambamba na kufundisha kwa juhudi zote ili ida...