WAENDESHA PIKIPIKI WADAI KUPIGWA FIMBO NA ASKARI
Baadhi ya waendesha pikpiki maarufu
kama bodaboda Manispaa ya Mpanda wamewalalamikia baadhi ya askari wa usalama
barabarani mkoani Katavi wanaowachapa viboko wanapokuwa wakisafirisha abiria.
Wamesema tabia ya askari hao imedumu
kuanzia mwaka 2016 ambapo licha ya kutoa malalamiko katika miktutano mbalimbali
ya hadhara inayoitishwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani bado
wameendelea kupigwa.
Kwa upande wake Afisa wa usalama
barabarani kutoka jeshi la polisi Mkoani Katavi Samweli Shigera amekanusha
waendesha bodaboda kupigwa na amewataka wanaotendewa vitendo hivyo waripoti
polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Mara kadhaa jeshi la Polisi kitengo
cha usalama barabarani limekuwa likituhumiwa kutumia nguvu kubwa kuwadhibiti
waendesha bodaboda wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments