BAVICHA WATOA NENO KWA SERIKALI KUHUSU AMANI NCHINI
Baraza la vijana la Chadema
(Bavicha) Mkoani Rukwa limeitaka Serikali kutumia gharama yoyote kulinda amani ya nchi inayoonesha
dalili ya kutoweka kutokana na kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya kinyama na
utekaji unaofanywa watu wasiojulikana.
Makamu
Mwenyekiti wa Bavicha,John Pambalu alisema hayo juzi wakati wa akifungua
kongamano la vijana lilolenga kuwapa elimu wanachama wake kuhusu wajibu
wao katika siasa za sasa ambalo liliandaliwa na Bavicha mkoa wa Rukwa.
Alisema
hali ya kisiasa hivi sasa hapa nchini ni tete kutokana kushamiri kwa vitendo
vya utekaji na mauaji ya kinyama yanayofanywa na watu wanaodaiwa kutojulikana
huku serikali ikiwa haijavalia njuga vya kutosha katika kudhibiti vitendo
hivyo.
Makamu
huyo mwenyekiti alisema imefika wakati sasa serikali kutumia gharama yoyote ili
kulinda amani ya taifa hili iliyoasisiwa na Baba wa taifa Mwl.Julius Nyerere
ambaye katika utawala wake na zile zilizopita hawakukubali kuona amani ikitiwa
doa.
Awali,Mwenyekiti
wa Bavicha mkoa wa Rukwa,Aida Khenan aliwataka vijana wa Chadema mkoani humo
kulitumia kongamano hilo kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto za
kisiasa ambazo zimekuwa zikiathiri ustawi wa vyama vya upinzani hapa nchini.
Khenan
ambaye pia mbunge wa viti maalumu mkoani Rukwa,alisema vijana hao wanapaswa
kutumia fursa ya kongamano hilo kubaini mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato
ili wajikwamue kiuchumia na hatimaye kuondokana na umasikini.
Wakati
huo huo amesema ili vijana washiriki kikamilifu katika siasa za mageuzi
wanapaswa wawe na nguvu ya kiuchumi hivyo makongamano kama hayo yanawapa fursa
ya kubaini mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato.
Habari zadi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments