WANAWAKE WAMZIKA MWANAMKE MWENZAO ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE KABLA NA BAADA YA KUFARIKI.
Wanawake wa mtaa wa Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,hatimaye wamefanya mazishi ya mwanamke mwenzao
Rosemary Robert Ismail makazi wa mtaa huo aliyefariki dunia siku sita
zilizopita baada ya kutelekezwa na mumewe Bw.Abdalla Ibrahim akiwa mgonjwa.
Wanawake hao wamesema wamefanya
mazishi jana baada ya kupata kibali cha jeshi la Polisi Mkoani Katavi
kinachowaruhusu kufanya hivyo baada ya ndugu zake kukosekana.
Katika hatua nyingine wanawake wanadai
kutishiwa maisha na Bw.Abdalla Ibrahim kwa madai kuwa wameripoti kifo cha
mwanamke mwenzao katika vyombo vya habari.
Kwa upande wa mjumbe wa serikali ya
Mtaa wa Mpanda Hotel Bi.Edita Nichoraus pamoja na mambo mengine amesema Bw.Abdalla
Ibrahim ataitishwa kuanzia kesho Machi 14 ili kujibu tuhuma za vitisho vya
maisha anavyovielekeza wa wanawake walioshiriki mazishi.
Rosemary Robert Ismail anadaiwa
kufariki Machi 7 mwaka huu na amezikwa juzi ambapo Bw.Abdalla Ibrahim awali
katika mazungumzo na Mpanda Radio alisema marehemu hakuwa mkewe.
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments