RAIS MAGUFULI AWAONYA TRA
Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza
Kamishna wa TRA,Waziri wa Fedha na katibu mkuu kwenda kuishughulikia Shirika la
Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kuacha tabia zake chafu za kuwaongezea raia
kodi za mapato pindi wanapokwenda kupata huduma hizo.
Dkt.Magufuli ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa anatoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi wa ajili ya ujenzi
wa reli ya kisasa ya 'Standard Gauge' katika eneo la Ihumwa,Dodoma ambapo awamu
ya kwanza ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017,katika maeneo ya PUGU, Jijini
Dar es Salaam.
Pamoja na hayo,Dkt. Magufuli
ameendelea kwa kusema "TRA muangalie kodi zenu mnazozitoza, inawezekana
nyingine ni kubwa mno kuliko miradi wanayotekeleza wananchi badala ya kuwa
motisha kwa walipa kodi inakuwa kero kwao na badala yake wanabuni njia ya
kukwepa kulipa kodi.
Kwa upande mwingine,Dkt. Magufuli
ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya mlipa mkodi kwa wananchi ili kuweza
kuwapa uelewa wanachi na waweze kulipa kodi kwa heshima kwa taifa lake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments