CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA HATIHATI KUSITISHA KUDAHILI WANAFUNZI
CHUO
cha ualimu cha Sumbawanga kilichopo mkoani Rukwa huenda kikasitisha kudahili
wanafunzi ajili ya kujiunga na chuo hicho baada ya Kanisa katoliki jimbo la
Sumbawanga kudai majengo yake baada ya serikali kutowapatia majengo mengine
kama walivyoahidiana.
Katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa |
Alisema
kipindi hicho alikuwepo Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Sumbawanga marehemu
Karolo Msakila ambaye aliombwa majengo hayo ili yatumike kama ofisi za mkoa huo
ambapo alikubali na kuiazima serikali na ofisi za mkoa huo zilikuwa hapo.
Ilipofika
mwaka 1989 serikali ya mkoa huo ukawa umejenga ofisi zake lakini haukuyarudisha
majengo hayo kwa mmiliki wake ambaye alikuwa anataka kufungua chuo cha kilimo na
badala yake serikali ilianzisha chuo cha ualimu bila makubaliano yoyote.
Baada
ya muda mrefu kanisa katoliki liliyahitaji majengo yake ambapo serikali ya mkoa
iliahidi kulipatia majengo yalikuwa yakitumika na kampuni ya ujenzi ya barabara
kwa kiwango cha lami kati ya Sumbawanga-Tunduma lakini hata hivyo
serikali ya mkoa huo haikulipa kanisa majengo hayo badala yake yakatumika
kuanzisha tawi la chuo cha Sayansi cha Mbeya(MUST).
Kutokana
na hali hiyo kanisa katoliki lilihoji kuhusu hatma ya majengo yao ambapo
serikali ya mkoa iliahidi tena kulipa majengo ya kambi ya ujenzi wa barabara ya
Sumbawanga-Mpanda yaliyopo katika eneo la Makutano mjini Sumbawanga, lakini pia
haikuwa hivyo baada ya serikali kuweka ofisi za Tanroad mkoa na hivyo kanisa
kukosa majengo hayo.
Baada
ya kushindikana mara mbili zote kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga lilikutana
na uongozi wa serikali ya mkoa ambapo lilisema halitaki tena kupewa majengo
mengine bali wanataka majengo yao kwa kuwa kanisa hilo limevumilia na kufikia
mwisho.
Kutokana
na kujuwa majengo hayo si mali ya serikali kwa muda mrefu yalikuwa hayafanyiwi
ukarabati mpaka hapo NACTE ilipotishia kukifunga chuo hicho kutokana na kuwa
kimechakaa, ndipo serikali ya mkoa ilipoliomba tena kanisa katoliki liwape muda
ambapo lilitoa miaka mitano wanafunzi hao wawe wameondoka katika majengo yao na
serikali ya mkoa iwe imejenga chuo chake na wakabidhi majengo kwa kanisa hilo
liendelee na matumizi waliyokusudia wakati yakijengwa.
Mkuu
wa Mkoa wangabo aliwaambia wajumbe wa kikao cha RCC serikali ya mkoa
imewasiliana na tasisi ya Jumuiya ya Maendeleo mkoani Rukwa (JUMARU) ambapo
imetoa ardhi katika kijiji cha Pito nje kidogo ya mji wa Sumbawanga ambapo
yalikuwa mashamba ya bega kwa bega yanayomilikiwa na kijiji hicho ambapo
serikali ya mkoa imeanza mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo
cha ualimu Sumbawanga.
Alisema
lengo la serikali ya mkoa ni kujenga chuo hicho na kwa kuwa eneo ni kubwa
kijengwe pia chuo kikuu ambacho kitamilikiwa na serikali ambacho kitakuwa makao
yake makuu mkoani Rukwa.
Baada
ya taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti huyo wa RCC, wajumbe wa kikao hicho
walishauri kuwa ni vizuri pia ukarabati ukaendelea kufanyika katika chuo hicho
kinachotumika hivi sasa kilichopo eneo la Kantalamba ili NACTE wasisitishe
kuwapangia wanafunzi kwa kua miaka mitano waliyo azimwa na kanisa hilo bado ni
kipindi kirefu.
Chanzo:Rukwa kwanza Bolg
Habari zadi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments