RUKWA BADO WALIA NA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA
MKOA wa Rukwa bado unakabiliwa na
upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo jumla ya vyumba 4,226
vinakitajika ili kumaliza tatizo hilo.
Afisa elimu mkoa huo Nestory Mroka
alisema mahitaji hayo yamekuwa yakisababisha mkoa huo kutopiga hatua katika
mafanikio ya elimu.
Alisema ili wanafunzi wafanye
vizuri katika masomo yao ni lazima kuwe na miundombinu mizuri,walimu wa kutosha,vitabu
pamoja na walimu lakini kama kuna mapungufu kati ya hayo mambo hata ufaulu hauwezi
kuwa mzuri.
Aidha Mroka alisema kutokana na
changamoto hizo jitihada za makusudi zinahitajika katika kulimaliza tatizo hilo
pamoja na mengine ili kuinua ufaulu wa wanufunzi katika shule za msingi pamoja
na sekondari ambapo mpaka sasa ufaulu katika kidato cha nne ni wastani wa
daraja la nne.
Wakati huo huo,Afisa elimu huyo
alisema yeye binafsi amejitahidi kuhakikisha anawasimamia walimu ili watimize
wajibu wao ipasavyo ikiwamo kuwepo kazini kwa muda mwafaka sambamba na
kufundisha kwa juhudi zote ili idara ya elimu iwe mfano wa kuigwa kwa kufanya
vizuri mkoani humo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa
Rukwa Joachim Wangabo aliziagiza halmashauri zote za mkoani humo kuhakikisha zinakuja
na mikakati ya kumaliza tatizo hilo pamoja na kwamba limeongezeka
baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya elimu bure.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa hivi
sasa serikali inajikita katika uchumi wa viwanda lazima pia kuhakikisha kuwa
elimu haibaki nyuma na mzizi wa kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza vizuri
katika elimu kwani huko ndiko watapatikana wataalamu watakao fanya kazi katika
viwanda hivyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments