AUWAWA KWA SABABU YA MASHAMBA YAKE MJUKUU WAKE AHUSISHWA

JESHI la Polisi mkoani  Rukwa,linawashikilia watu sita akiwemo mjukuu aliyekubalichukua hongo Shilingi milioni moja na kukubali babu yake auawe kwa kupigwa rungu kichwani kutokana na ugomvi wa ardhi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa,George Kyando alisema jana kuwa tukio la kuuawa kwa mzee huyo aliyefahamika kwa jina la Paul Kisiwa (72) mkazi wa kijiji cha Ng'ongo lilitokea machi 3 nyakati za jioni kwenye kijiji cha Kifinga Kata ya Mtowisa wilaya Sumbawanga.
Taarifa kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Diwani wa Kata ya Mtowisa, Edger Malinyi, zilieleza kuwa baada ya kuuawa kwa mzee huyo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM ngazi ya kata alizikwa kinyemela shambani kwake.
Inaelezwa kuwa taarifa za kupotea mzee huyo zilianza kuzagaa ndipo ndugu wa marehemu pamoja na majirani  wakishirikiana na polisi walianza kuchunguza tukio hilo ambapo ilipofika machi 8 mwaka huu,watu hao walimbana mjukuu wa mzee huyo aitwaye John Kisiwa (22) ambaye alikiri kushiriki kupanga njama za kumuua babu yake kwa ujira wa Shilingi 1,000,000.
Diwani huyo,alisema kijana huyo alipanga njama ya mauaji hayo na wenzake ambao walikuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na mzee huyo ambaye awali aliwakodisha watu hao shamba la ekari zaidi 15 kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Alisema baadaye aliwanyang'anya shamba hilo na kuamua kulilima  yeye mwenyewe kitendo kilichowauzi watuhumiwa  hao ambao walijikuta wakiingia katika mgogoro wa kugombea eneo hilo, hali ilisababisha waandae mipango ya kumuua mzee huyo.
Inadaiwa kuwa  siku ya tukio la mauaji hayo, watu hao walimvamia mzee huyo akiwa katika  shambani lake hilo, na kisha kumpiga na rungu kichwani ambapo alianguka na kufariki dunia papo hapo.
Diwani Malinyi alisema baada ya kumuua mzee huyo walichimba shimo shambani humo na kumfukia ili kupoteza ushahidi hali iliyobainika baada ya mjukuu wake kubanwa na kueleza ukweli hivyo polisi walifukua eneo hilo na kukuta mwili wa mzee huyo.
Kamanda Kyando aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa kuwa ni Kela Lubinza (15), Chani Lubinza (29),Simba Lubinza (16)  wote wakiwa ni ndugu wa familia moja pia Deshi Mihambo (40) na Muli Sabini (21) ambao ni majirani wa wanafamilia hao.
Alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA