Posts

Showing posts from April 6, 2018

RAIS MAGUFULI ATUMBUA MKURUGENZI

Image
Rais Dkt.John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma,Mohamed Maja kuanzia leo kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuisababishia halmashauri hiyo upotevu mkubwa wa fedha za serikali. Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mussa Iyombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma. Amesema utenguzi huo umefanyika ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi juu ya tuhuma hizo. Iyombe amesema tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa utendaji katika ofisi ya mkurugenzi huyo imebaini baadhi ya fedha zinapotea mikononi mwa watu na mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti. Wakati huo huo Iyombe amesema Mkurugebnzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi. Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege, amewataka wenyeviti wa halmashauri kote nchini kuzingatia mafunzo waliyopewa na uongozi wa chuo cha serikali za mitaa hombolo ili wawe mabalozi bora katika maen...

RAIS MAGUFULI AZINDUA UKUTA KUZUNGUKA MADINI YA TANZANIATE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amezindua ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro mkoani Manyara uliojengwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa madini na ukwepaji wa kodi. Ukuta huo wenye urefu wa kilometa 24.5 umejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5 na Milioni 646 ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa tarehe 20 Septemba,2017 na Mhe.Rais Magufuli alipokuwa akizindua barabara ya KIA – Mirerani. Mhe.Rais Magufuli ameipongeza JWTZ kwa kukamilisha kazi hiyo kwa haraka na kwa gharama nafuu na amewapongeza maafisa,askari na vijana 2,356 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki katika ujenzi kwa uzalendo wao na kujituma ili kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa Taifa. Mhe.Rais Magufuli amelikubali ombi la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na ameagiza vijana wa JKT walioshiriki katika ujenzi wa ukuta huo waajiriwe katika vyomb...

WANAFUNZI 11 WAPATA MIMBA KATAVI

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Francis Nzyungu amesema wanafunzi wapatao 11 katika shule zake wamepata ujauzito na kukatiza kuendelea na masomo katika kipindi cha mwaka 2017. Nzyungu ameibainisha hali hiyo juzi wakati akiwasilisha taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi kupitia kikao cha wadau wa elimu kilichokuwa kimeandaliwa maalumu ili kujadili na kutathmini hali ya ufaulu wa wanafunzi Mkoani Katavi katika mitihani ya taifa kwa shule za msingi na sekondari. Amesema kati ya mimba hizo 11 zilizoripotiwa kwa katibu tawala wa Mkoa wa Katavi,mimba 3 zimeshafikishwa polisi huku mimba nyingine zikishughulikiwa katika ngazi ya maafisa watendaji wa kata na mitaa ili kutafuta ufumbuzi. Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Paulina Wilison wa Mpanda Girls Sekondari,na Philbeti Mapunda mwenyekiti wa kamati ya shule ya sekondari Shanwe ambaye pia alikuwa miongoni mwa wadau wa elimu malezi mabaya,umaskini pamoja na ukosefu wa mabweni hasa kwa watoto w...

HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA KUWAWEZESHA WATU WENYE ULEMAVU MWAKA FEDHA 2018/2019

Image
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imesema kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 itaanza kutoa asilimia 2 ya mikopo kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Hatua hiyo imebainishwa na Kaimu Mkurugenzi   halmashauri hiyo Samson Medda ambapo amesema katika mgawanyo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri wanawake watakuwa wanapata asilimia 4 na vijana asilimia 4 na 2 kwa watu wenye ulemavu. Kwa mjibu wa Medda,mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu,halmashauri imetoa fedha kutoka katika mapato ya ndani   kiasi cha shilingi milioni 119 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake   na vijana. MAENEO AMBAYO HALMASHAURI ILIWEZESHA 1.Kikundi cha vijana Kata ya Majalila cha kufyatua tofali kilipewa pesa 2.Kikundi cha wanawake cha Sibwesa kinachoseketa mashuka na vikoi kilipewa fedha 3.Mashine ya kukoboa na kusaga mahindi-kata ya Kabungu 4.Kiwanda cha Chaki na Sabuni-kata ya Ifukutwa 5.Pikipiki 11 zilinunuliwa na kusambazwa vijana ambapo 4-zilipelekwa...