WANAFUNZI 11 WAPATA MIMBA KATAVI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Francis Nzyungu amesema wanafunzi
wapatao 11 katika shule zake wamepata ujauzito na kukatiza kuendelea na masomo
katika kipindi cha mwaka 2017.
Nzyungu ameibainisha hali hiyo juzi wakati
akiwasilisha taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi kupitia kikao cha wadau wa
elimu kilichokuwa kimeandaliwa maalumu ili kujadili na kutathmini hali ya
ufaulu wa wanafunzi Mkoani Katavi katika mitihani ya taifa kwa shule za msingi
na sekondari.
Amesema kati ya mimba hizo 11
zilizoripotiwa kwa katibu tawala wa Mkoa wa Katavi,mimba 3 zimeshafikishwa
polisi huku mimba nyingine zikishughulikiwa katika ngazi ya maafisa watendaji wa
kata na mitaa ili kutafuta ufumbuzi.
Kwa upande wao wanafunzi akiwemo
Paulina Wilison wa Mpanda Girls Sekondari,na Philbeti Mapunda mwenyekiti wa
kamati ya shule ya sekondari Shanwe ambaye pia alikuwa miongoni mwa wadau wa
elimu malezi mabaya,umaskini pamoja na ukosefu wa mabweni hasa kwa watoto wa
kike bado ni vyanzo vikubwa vinavyochangia mimba kwa wanafunzi walio katika
umri mdogo.
Hata hivyo serikali imekuwa ikiagiza
kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya wanaosababisha mimba kwa wazazi
pamoja na wazazi au walezi wanaowaoza watoto wao kwa kigezo cha kupata mahali.
Mkoa wa Katavi ndiyo unaoongoza kwa
mimba za utotoni kati ya mikoa ya Tanzania kwa kuwa na asilimia 45 ambapo wengi
wao wanakuwa katika umri wa kuwa shuleni.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments