RAIS MAGUFULI ATUMBUA MKURUGENZI
Rais
Dkt.John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa
mkoani Dodoma,Mohamed Maja kuanzia leo kutokana na kushindwa kusimamia
ukusanyaji wa mapato na kuisababishia halmashauri hiyo upotevu mkubwa wa fedha
za serikali.
Hayo
yamebainishwa na Katibu mkuu wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za
mitaa Tamisemi Mussa Iyombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini
Dodoma.
Amesema
utenguzi huo umefanyika ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi juu ya tuhuma
hizo.
Iyombe
amesema tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa utendaji katika ofisi ya
mkurugenzi huyo imebaini baadhi ya fedha zinapotea mikononi mwa watu na
mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti.
Wakati huo huo Iyombe amesema Mkurugebnzi huyo kwa
sasa yupo chini ya uchunguzi.
Kwa
upande wake,Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege, amewataka wenyeviti wa
halmashauri kote nchini kuzingatia mafunzo waliyopewa na uongozi wa chuo cha
serikali za mitaa hombolo ili wawe mabalozi bora katika maeneo yao.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments