Posts

Showing posts from April 1, 2018

ASKOFU SHOO ASEMA WANAOPOTOSHA UKWELI WARAKA WA MAASKOFU KKKT NI WAJINGA

Image
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Fredrick Shoo,amesema wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa kuupaka matope ni wajinga. Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka katika ibada maalumu ya kusherekea sikukuu hiyo. Amesema kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kupotosha waraka  wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope kwa malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni wajinga. Askofu Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za kujaribu kuuzima ukweli ulipo katika waraka huo na wao hawajali kuhusu hilo bali watasimamia ukweli zaidi.   Habari zaidi ni  WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

RAIS AUNGANA NA WAKRISTO SIKUKUU YA PASAKA ATAKA WATANZANIA WAISHI KWA UPENDO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka. Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa amesema rais ameshiriki misa iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Padre Venance Tegete. Akizungumza baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa salamu,Mhe.Rais Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Pasaka. Aidha rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa. Mhe.Rais Magufuli aliongozana na Mkewe Mhe.Mama Janeth Magufuli. Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM