RAIS AUNGANA NA WAKRISTO SIKUKUU YA PASAKA ATAKA WATANZANIA WAISHI KWA UPENDO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa
Takatifu ya sikukuu ya Pasaka.
Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa
amesema rais ameshiriki misa iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph,
Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu
Joseph Padre Venance Tegete.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa
salamu,Mhe.Rais Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Pasaka.
Aidha rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi
kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.
Mhe.Rais Magufuli aliongozana na Mkewe Mhe.Mama Janeth Magufuli.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments