ASKOFU SHOO ASEMA WANAOPOTOSHA UKWELI WARAKA WA MAASKOFU KKKT NI WAJINGA
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Fredrick Shoo,amesema
wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa kuupaka matope
ni wajinga.
Askofu
Shoo ametoa kauli hiyo leo katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini
mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka katika ibada maalumu ya
kusherekea sikukuu hiyo.
Amesema
kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia nguvu
nyingi kupotosha waraka wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope kwa
malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni wajinga.
Askofu
Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo
watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za kujaribu
kuuzima ukweli ulipo katika waraka huo na wao hawajali kuhusu hilo bali
watasimamia ukweli zaidi.
Comments