MKOA WA KATAVI WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI.
Na.Issack Gerald-Katavi MKOA wa Katavi umeshauriwa kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na katika maeneo ya makazi na hifadhi. Ushauri huo umetolewa jana na Waziri mkuu mstaafu Mh, Mizengo Pinda katika kikao cha Kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini Mpanda.