MKOA WA KATAVI WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI.
Na.Issack
Gerald-Katavi
MKOA
wa Katavi umeshauriwa kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji
na katika maeneo ya makazi na hifadhi.
Ushauri
huo umetolewa jana na Waziri mkuu mstaafu Mh, Mizengo Pinda katika kikao cha
Kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini
Mpanda.
Amesema
migogoro ya ardhi inasababishwa na ongezeko la watu wanaohamia ndani ya mkoa wa
Katavi kutoka mikoa mingine nchini bila kufuata maelekezo ya waraka wa serikali
wa mwaka 2000.
Waziri
mkuu mstaafu Pianda ameshauri mjadala huo upewe nafasi kubwa na kila
halmashauri mkoani Katavi itoe mwongozo wa matumizi ya ardhi na kutoa taarifa
katika ngazi ya mkoa ili ufumbuzi wa tatizo hilo uweze kupatikana.
Kikao
hicho kimeshirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo mkoani Katavi wakiwemo wabunge saba wakiwemo watano wanaochaguliwa na wananchi.
Migogoro mingi katika Mkoa wa Katavi
imekuwa ikiibuka ikihusisha wakulima na wafugaji,maafisa kuuza kiwanja kwa mtu
zaidi ya mmoja,wakulima kuingia katika eneo la hifadhi za mkoa wa Katavi.
Comments