Posts

Showing posts from April 3, 2018

VIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI WA CHADEMA WAACHIWA HURU

Image
Wanasiasa saba wa upinzani wakiwemo viongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema wameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwapatia dhamana wanasiasa sita wiki iliyopita lakini waliendelea kubaki rumande kwa kuwa hawakuwepo mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana yao. Mtuhumiwa wa saba,Halima Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe,aliongezwa leo katika orodha ya washtakiwa na kufanya jumla ya washtakiwa kuwa saba. Washtakiwa wote wanakabiliwa na mshtaka 8 ambayo ni pamoja na kukusanyika na kufanya maandamano kinyume na sheria pamoja na kutoa maneno yanayoweza kusababisha vurugu na chuki miongoni mwa jamii. Kwa msingi huo,Halima Mdee pia amepatiwa dhamana kwa masharti kama yale yale ya wenzake wa awali ambayo ni pamoja na wadhamini wawili,kila mdhamini asaini bondi ya shilingi za Kitanzania milioni 20 na kukabidhi vitambulisho vinavyotambulika kisheria. Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi hiyo amet...

MATUKIO YA UHALIFU NI 0 WAKATI WA SHEREHE ZA PASAKA MKOANI KATAVI

Image
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema hakuna uhalifu wowote ulijitokeza katika kipindi cha sikukuu ya pasaka. Kamanda Nyanda amebainisha hatua hiyo wakati akizungumzia hali ya ulinzi na usalama katika sherehe za pasaka kwa mwaka 2018 ambazo wakaristo kote duniani husherehekewa sikukuu hiyo. Aidha amesema hakuna matukio ya vifo wala majeruhi yaliyotokana na ajali za barabarani ambazo zimesababishwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani. Hata hivyo,mbali na kuwapongeza wananchi wa mkoa wa Katavi kwa kuthamini usalama na kusherehekea kwa amani na utulivu,amesema jeshi la polisi litaendelea kudhibiti viashiria vyovyote vy akiuharifu ili wananchi waendelee kuwa salama pamoja na mali zao. Katika kipindi cha Januari mpaka Machi 2018,matukio kadhaa ya uhalifu yalitokea mkoani Katavi ikiwemo matukio ya Januari 27 kata ya Ugalla na Februari 25 mwaka huu mgodi wa Islamilomo wilayani Mpanda ambapo watu wawili walikufa kwa kupigwa risasi na majambazi ny...

NIDA YASEMA KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA NI BURE

Image
Kaimu msajili wa vitambulisho vya Taifa Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi Bi.Nasra Said amesema hakuna gharama zozote ambazo wananchi wanatakiwa kulipia ili kujiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha taifa. Bi.Nasra amesema wananchi wanapokwenda kujiandikisha wanatakiwa wawe na nakala mojawapo kati ya kitambulisho cha Mpiga kura,cheti cha kuzaliwa au cheti cha shule. Badhi ya wananchi wilayani Tanganyika wakiwemo Bw.Emmanuel Adiriano na Samweli John wamelalaka kulipishwa fedha mpaka shilingi 1000 kwa ajili   ya kujiandikisha huku wengine wakisema hawana elimu yoyote kuhusu vitambulisho hivyo vya taifa na kuhofia kukosa haki yao ya msingi. Utaratibu wa kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilianzishwa mwaka 1968 katika kikao kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda na Zambia. Kwa mjibu wa maelezo ya serikali ya Tanzania,vitambulisho hivyo vinalenga kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingat...