NIDA YASEMA KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA NI BURE
Kaimu msajili wa vitambulisho vya
Taifa Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi Bi.Nasra Said amesema hakuna gharama zozote
ambazo wananchi wanatakiwa kulipia ili kujiandikisha kwa ajili ya kupata
kitambulisho cha taifa.
Bi.Nasra amesema wananchi wanapokwenda
kujiandikisha wanatakiwa wawe na nakala mojawapo kati ya kitambulisho cha Mpiga
kura,cheti cha kuzaliwa au cheti cha shule.
Badhi ya wananchi wilayani Tanganyika
wakiwemo Bw.Emmanuel Adiriano na Samweli John wamelalaka kulipishwa fedha mpaka
shilingi 1000 kwa ajili ya kujiandikisha
huku wengine wakisema hawana elimu yoyote kuhusu vitambulisho hivyo vya taifa
na kuhofia kukosa haki yao ya msingi.
Utaratibu wa kuanzisha Vitambulisho
vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilianzishwa
mwaka 1968 katika kikao kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za
Tanzania,Kenya,Uganda na Zambia.
Kwa mjibu wa maelezo ya serikali ya
Tanzania,vitambulisho hivyo vinalenga kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia
Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne kwa kuwapatia raia wake vitambulisho vya
taifa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments