MATUKIO YA UHALIFU NI 0 WAKATI WA SHEREHE ZA PASAKA MKOANI KATAVI
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi ACP Damas Nyanda amesema hakuna uhalifu wowote ulijitokeza katika
kipindi cha sikukuu ya pasaka.
Kamanda Nyanda amebainisha hatua hiyo
wakati akizungumzia hali ya ulinzi na usalama katika sherehe za pasaka kwa
mwaka 2018 ambazo wakaristo kote duniani husherehekewa sikukuu hiyo.
Aidha amesema hakuna matukio ya vifo
wala majeruhi yaliyotokana na ajali za barabarani ambazo zimesababishwa na
ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.
Hata hivyo,mbali na kuwapongeza
wananchi wa mkoa wa Katavi kwa kuthamini usalama na kusherehekea kwa amani na
utulivu,amesema jeshi la polisi litaendelea kudhibiti viashiria vyovyote vy
akiuharifu ili wananchi waendelee kuwa salama pamoja na mali zao.
Katika kipindi cha Januari mpaka
Machi 2018,matukio kadhaa ya uhalifu yalitokea mkoani Katavi ikiwemo matukio ya
Januari 27 kata ya Ugalla na Februari 25 mwaka huu mgodi wa Islamilomo wilayani
Mpanda ambapo watu wawili walikufa kwa kupigwa risasi na majambazi nyakati za
usiku katika matukio hayo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa na mali kadhaa
kuibwa.
Mbali na matukio hayo vibaka nao
wamekuwa wakitajwa kuwa kero kwa wakazi wengi kutokana na wizi wa mali za
majumbani hasa ukatwaji wa nyavu madirishani na kuiba mali kama vile simu,radio,tv,sola
za umeme na hata komputa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments