VIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI WA CHADEMA WAACHIWA HURU
Wanasiasa saba wa upinzani wakiwemo
viongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema wameachiwa huru
baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
iliwapatia dhamana wanasiasa sita wiki iliyopita lakini waliendelea kubaki
rumande kwa kuwa hawakuwepo mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana yao.
Mtuhumiwa wa saba,Halima Mdee ambaye
pia ni Mbunge wa Kawe,aliongezwa leo katika orodha ya washtakiwa na kufanya
jumla ya washtakiwa kuwa saba.
Washtakiwa wote wanakabiliwa na
mshtaka 8 ambayo ni pamoja na kukusanyika na kufanya maandamano kinyume na
sheria pamoja na kutoa maneno yanayoweza kusababisha vurugu na chuki miongoni
mwa jamii.
Kwa msingi huo,Halima Mdee pia
amepatiwa dhamana kwa masharti kama yale yale ya wenzake wa awali ambayo ni
pamoja na wadhamini wawili,kila mdhamini asaini bondi ya shilingi za Kitanzania
milioni 20 na kukabidhi vitambulisho vinavyotambulika kisheria.
Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri
anayesikiliza kesi hiyo ametaja tarehe 16 April kuwa ndio siku ya Kusikilizwa
kwa awali kwa kesi ya wanasiasa hao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments