MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA ABWAGA MANYANGA
Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Bw.Theophil Makunga amejiuzulu nafasi hiyo. Taarifa ya kujizulu kwa Bw.Makungu imetolewa leo katika vyombo vya habari na Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) na kueleza kuwa mwenyekiti huyo amejiuzulu tangu jana. Kwa mjibu wa TEF,Bw.Makungu amechukua hatua hiyo kwa kutumia uhuru wake binafsi kama mwanachama hai ambapo mkutano wa dharura umefanyika leo na kuridhia kujiuzulu kwake. Pamoja na jukwaa kusema litakosa busara za Bw.Makungu katika taaluma ya habari pia limemtakia kila la heri katika majukumu yake mengine. Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM